Huduma za uazimaji [Matini] za Maktaba
Unaweza kuazima matini ili kutumia ndani na nje ya maktaba kwa muda maalumu. Ni wafanyakazi wa Wizara ya Fedha tu wanaoruhusiwa kuazima matini. Watumiaji wengine kutoka nje ya Wizara hawaruhusiwi kuazima matini. Wafanyakazi wetu wa Huduma kwa Wateja watakuwepo kwenye vituo vya huduma, muda wa kazi.
Huduma Inayotolewa:
- Idadi ya vitabu vinavyoazimwa kwa mtu [mmoja] = vitabu 3.
- Muda mrefu [zaidi] kwa mtu kukaa na vitabu [alivyoazima] = siku 14.
- Huduma za uazimaji ni kwa wafanyakazi wa WFM pekee.
Tunachoweza kufanya:
Tunatoa huduma ya uazimishaji wa matini za maktaba, pamoja na usaidizi wa kina wa utafutaji wa matini hizo. Idadi kubwa ya rasilimali za kanzidata zinapatikana pia mtandaoni.
Huduma hii inatolewa kwa:
Huduma zetu za uazimishaji zinapatikana kwa watumishi wa MoFP na wananchi wa ujumla, Hata hivyo ikiwa wewe si mtumishi wa wizara vikwazo vitaweza kutumika katika uazimishaji.
Jinsi ya kutumia:
Tembelea mifumo ya Maktaba (Opac au repository) ili kuona machapisho yanayopatikana katika Maktaba yetu, kwa usaidizi zaidi tembelea Ofisi yetu ya Maktaba wakati wa saa za kazi ili kuazimisha matini.
Kuongeza muda wa kutumia
Unaruhusiwa kuongeza muda wa matini ulizoazimisha kutoka kwa maktaba, ikiwa hakuna mtumishi mwingine aliyeomba matini hiyo.
.
Namna ya kukuhudumia:
Kwa msaada zaidi wasiliana na wafanyakazi wa Maktaba .